1. Acha kupoteza wakati kwenye tovuti za ponografia na nyinginezo kam hizo.
2. Usifuate umati wa watu (mkumbo), fuata njia yako mwenyewe. Fanya kile unachopenda.
3. Punguza kutumia muda mwingi katika tovuti za kijamii.
4. Usijifunze tu kutoka kwa hadithi za mafanikio, jifunze kutoka kwa hadithi za kufeli "kwanini walishindwa '? Pata na ujifunze kutoka kwao.
5. Jaribu kuwa muongeaji mzuri kwenye mikutano ya ofisi. Nina amini, itakupeleka kwenye kazi yenye mafanikio.
6. Dhibiti hisia zako na jaribu kuwa makini na tayari kwa hali yoyote ile.
7. Pigania maono yako na ndoto zako. Mafanikio yataanza kukufuata.
8. Jaribu kuwa mbunifu. Unapaswa kuwa na diary ili kuorodhesha maoni yako ya ubunifu.
9. Tengeneza video nzuri na yenye tija ambayo inahusiana na taaluma yako na ipakie kwenye akaunti yako ya YouTube ama sehemu nyingine.
10. Kuwa mtu wa vitendo. Maisha yatakuwa rahisi.
11. Unapofanya kazi, tumia simu yako maalum tu kwa kupiga simu, sio kwa sababu nyingine yoyote kama uchezaji magemu, kuangalia taarifa tofauti n.k.
12. Andaa/tengeneza utaratibu wa kila siku na uufuate kwa uhakika.
13. Jifunze lugha tofauti na lugha yako mama (5-6).
14. Soma vitabu vya kukupa hamasa ya mafanikio kama The Power of Now-Echkart Tolle, The Monk Who Sold His Ferrari-Robin Sharma, Outliers-Malcolm Gladwell.
15. Zingatia kazi yako na ufanye mipango yako badala ya kujihusisha katika mahusiano ya kufadhaisha (jiepushe na msongo wa mawazo).
16. Fanya kazi na watu bora katika taaluma yako na ujifunze kutoka kwao.
17. Daima fika/wahi ofisini kwa wakati.
18. Acha kufuatilia, kuvutia na kufurahisha watu wa jinsia tofauti (au jinsia yako).
19. Usiwe mpenda mali.
20. Usitegemee chochote kutoka kwa mtu yeyote.
21. Daima jaribu kutoa juhudi zako kwa 100%.
22. Jenga tabia zenye tija na nguvu.
23. Kariri majina ya rafiki, wafanya kazi wenzako na wasaidizi.
24. Elewa siasa za ofisini.
25. Kuwa wa kushangaza na kamwe usiseme kila kitu kuhusu wewe.

0 Comments